Algeria: Kamwe hatutachukua mkopo wa kigeni licha ya matatizo yetu
Waziri Mkuu wa Algeria amesema kuwa, kuchukua mkopo wa kigeni ni mstari mwekundu wa serikali yake.
Abdul Majeed Taboun ameyasema hayo katika kikao na mkuu wa Jumuiya ya Waajiri na Wafanyakazi wa nchi hiyo na kuongeza kuwa, licha ya kwamba nchi hiyo inakabiliwa na matatizo mengi ya kifedha hasa baada ya kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa, lakini serikali haitochukua mkopo wa kigeni. Majeed Taboun amefafanua kuwa, Rais Abdelaziz Bouteflika wa nchi hiyo amepiga marufuku nchi yake kuchukua mkopo kutoka nje hadi pale taifa litakapokuwa halikabiliwi na hatari yoyote.
Waziri Mkuu wa Algeria amesema kuwa, nchi hiyo inataka kuwa moja ya nchi ambazo zinastawi kiuchumi kwa kzualisha bidhaa za aina mblimbli na katika uwanja huo imeazimia kutekeleza mipango ya uwekezaji kwa njia ya busara. Abdul Majeed Taboun amesisitiza kuwa, soko la Algeria ni lazima lijae bidhaa zinazozalishawa ndani nchi na kwamba ikiwa uzalishaji wa ndani utaimarika, basi nchi hiyo haitoruhusu tena bidhaa za kigeni kuingia ndani ya nchi.