China kuisaidia Gambia baada ya kukata uhusiano na Taiwan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i32592-china_kuisaidia_gambia_baada_ya_kukata_uhusiano_na_taiwan
China imeahidi kuipa msaada Gambia baada ya nchi hiyo ya Kiafrika kukata uhusiano rasmi na serikali tya Taiwan.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 02, 2017 08:10 UTC
  • China kuisaidia Gambia baada ya kukata uhusiano na Taiwan

China imeahidi kuipa msaada Gambia baada ya nchi hiyo ya Kiafrika kukata uhusiano rasmi na serikali tya Taiwan.

Katika mkutano mjini Beijing, Wang Yi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa China amemuambia mwenzake wa Gambia Ousainou Darboe, ambaye yuko mjini humo kuwa, China iko tayari kuisadia Gambia katika nyuga za miundomsingi, kilimo, utalii na sekta nyinginezo.

Hata hivyo waziri huyo wa China hajatoa maelezo zaidi kuhusu muda, kiwango cha msaada na ushirikiano kati ya nchi yake na Gambia. 

China inaitambua Taiwan ambayo mwaka 1949 ilijitenga na nchi hiyo baada ya vita vya ndani, kuwa ni sehemu ya ardhi yake.

Rais wa Gambia, Adama Barrow na wafadhili wa Ulaya

Haya yanajiri wiki mbili baada ya China kutuma meli za kivita katika kituo chake cha kwanza cha kijeshi nje ya nchi ambacho kiko nchini Djibouti katika eneo la Pembe ya Afrika, ikiwa ni katika jitihada za nchi hiyo ya Asia kuimarisha ushawishi wake wa kiuchumi na kijeshi katika bara hilo.

Februari mwaka huu, Neven Mimica, Kamishna wa Ushirikiano na Ustawi wa Umoja wa Ulaya alisema kuwa, umoja huo utaisaidia serikali ya Gambia msaada wa kiasi cha Euro milioni 75, utakaosaidia kutatua matatizo ya chakula, ukarabati wa barabara na kuanzisha fursa za ajira nchini humo.