Kamanda wa jeshi la Libya anayesakwa na ICC akamatwa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i33290-kamanda_wa_jeshi_la_libya_anayesakwa_na_icc_akamatwa
Maafisa usalama mashariki mwa Libya wamemtia nguvuni kamanda wa Jeshi la Taifa la Libya (LNA), siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutoa waranti wa wa kumatawa kwake kwa tuhuma za kuua makumi ya wafungwa
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 18, 2017 03:36 UTC
  • Kamanda wa jeshi la Libya anayesakwa na ICC akamatwa

Maafisa usalama mashariki mwa Libya wamemtia nguvuni kamanda wa Jeshi la Taifa la Libya (LNA), siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutoa waranti wa wa kumatawa kwake kwa tuhuma za kuua makumi ya wafungwa

Hata hivyo taarifa ya Jeshi la Taifa la Libya (LNA) linalodhibiti maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika haijaeleza iwapo itamkabidhi kamanda huyo kwa ICC au la.

Waendesha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai Jumanne iliyopita walisema, Mahmoud al-Werfalli aliua na kuamuru mauaji ya wafungwa katika matukio saba yakiwemo ya kuua wafungwa 33 miezi ya Juni na Julai mwaka huu katika jela iliyoko karibu na mji wa Benghazi. 

Al-Werfalli (kushoto)

Umoja wa Mataifa pia ulilitaka Jeshi la Taifa la Libya kumsimamisha kazi Mahmoud al-Werfalli baada ya kusambazwa mkanda wa video uliomuonesha kamanda huyo wa jeshi la Libya akiwapiga risasi na kuwaua watu watatu waliokuwa wamepiga magoti na kuangalia ukutani wakiwa wamefungwa mikono nyuma ya migongo yao. 

Itakumbukwa kuwa, mwaka 2011 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliipa Mahakama ya Kimataifa Jinai (ICC) idhini ya kufuatilia na kushughulikia jinai za kivita zinazofanyika nchini Libya.