Aliyefanya mashambulizi ya kigaidi Algeria atambuliwa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i33863-aliyefanya_mashambulizi_ya_kigaidi_algeria_atambuliwa
Duru za usalama za Algeria zimetangaza habari ya kujulikana utambulisho wa mtu aliyefanya shambulio la kujiripua kwa bomu kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 01, 2017 22:00 UTC
  • Aliyefanya mashambulizi ya kigaidi Algeria atambuliwa

Duru za usalama za Algeria zimetangaza habari ya kujulikana utambulisho wa mtu aliyefanya shambulio la kujiripua kwa bomu kaskazini mwa nchi hiyo.

Duru hizo zimetangaza kuwa, mtu aliyefanya shambulio la kujiripua kwa bomu katika mji wa Tiaret wa kaskazini mwa Algeria juzi Alkhamisi anajulikana kwa jina la Boucetta Ben Aissa, maarufu kwa jina la Abu Jihad.

Maafisa usalama wa Algeria wanasema kuwa, kuna mtu mwingine alishirikiana na Ben Aissa katika shambulio hilo na anaendelea kusakwa na polisi. Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh limetangaza kuhusika na shambulio hilo.

Maafisa usalama wa Algeria baada ya kutokea shambulio la kigaidi mjini Tiaret siku ya Alkhamisi

 

Kabla ya hapo, vyombo vya habari vya Algeria vilikuwa vimetangaza habari ya kuweko taarifa za kijasusi zinazoonesha kuwa magaidi walikuwa wamepanga kufanya mashambulio katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo na kwamba polisi walikuwa wamewekwa katika hali ya tahadhari kubwa.

Juzi Alkhamisi, gaidi mmoja wa genge la wakufurishaji la ISIS alikusudia kujiripua katika jengo la ofisi ya usalama huko Tiaret, kaskazini mwa Algeria, hata hivyo maafisa usalama walimzuia kufika kwenye jengo hilo akaamua kujiripua na kuua polisi watatu.