UN yapasisha azimio la vikwazo dhidi ya Mali
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio dhidi ya shakhsia au makundi yanayokwamisha mchakato wa kurejesha amani nchini Mali.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio hilo kwa kura nyingi ambalo linaandaa uwanja wa kuwekewa vikwazo shakhsia au makundi yanayokwamisha utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Mali yaliyosainiwa mwaka 2015. Azimio hilo la Baraza la Usalama ambalo linaungwa mkono na Ufaransa, litawahusu pia shakhsia au makundi yanayozuia kutolewa misaada ya kibinadamu huko Mali na kukiuka sheria kuhusu masuala ya kibinadamu.
Francois Delattre, mwakilishi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa amesema baada ya kupigwa kura za kuunga mkono azimio hilo kuhusiana na Mali kwamba, azimio hilo ni ujumbe mzito kwa wale wote wanaoendelea kukwamisha kurejeshwa amani huko Mali.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa pia umeunda kamati ya vikwazo inayozijumuisha nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama ili kuwatambua watu au taasisi zinazopasa kuorodheshwa katika faharasa ya vikwazo.