UN yaitaka Togo kukidhi matakwa halali ya wananchi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34089-un_yaitaka_togo_kukidhi_matakwa_halali_ya_wananchi
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Togo ameitaka serikali ya nchi hiyo iwatimizie wananchi matarajio waliyonayo wakati polisi wa nchi hiyo wakiripotiwa kukabiliana na waaandamanaji wanaotaka kuhitimishwa utawala wa kifamilia wa miaka hamsini nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 08, 2017 14:24 UTC
  • UN yaitaka Togo kukidhi matakwa halali ya wananchi

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Togo ameitaka serikali ya nchi hiyo iwatimizie wananchi matarajio waliyonayo wakati polisi wa nchi hiyo wakiripotiwa kukabiliana na waaandamanaji wanaotaka kuhitimishwa utawala wa kifamilia wa miaka hamsini nchini humo.

Mohamed Ibn Chambas pia ametoa wito wa kuwepo utulivu na kusema kuwa anataraji kwamba chama tawala nchini Togo na vyama vya upinzani vitafikia makubaliano. 

Maelfu ya wananchi wa Togo leo waliandamana kwa siku ya tatu mfululizo katika mitaa ya miji mkuu wa nchi hiyo wakimtaka Rais Faure Gnassingbe ang'atuke madarakani, hatua ambayo imetajwa kuwa ni changamoto kubwa kwa familia hiyo iliyoko madarakani nchini Togo kwa muda wa miaka hamsini. Faure Gnassingbe amekuwa katika hatamu za uongozi tangu kufariki dunia baba yake mwaka 2005.  

Rais Faure Gnassingbe wa Togo 

Polisi wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji ambao walikuwa wakichoma moto tairi za magari katika ngome ya upinzani katika eneo la Be katika mji mkuu wa nchi hiyo, Lome.