Djibouti yakosoa namna ya ufuatiliaji kadhia ya Syria katika nchi za Kiarabu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34291-djibouti_yakosoa_namna_ya_ufuatiliaji_kadhia_ya_syria_katika_nchi_za_kiarabu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti amesema kuchunguzwa kadhia ya Syria katika nchi za Ulaya ni ishara ya udhaifu katika nchi za Kiarabu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 13, 2017 03:01 UTC
  • Djibouti yakosoa namna ya ufuatiliaji kadhia ya Syria katika nchi za Kiarabu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti amesema kuchunguzwa kadhia ya Syria katika nchi za Ulaya ni ishara ya udhaifu katika nchi za Kiarabu.

Kwa mujibu wa gazeti la Al Youm al Sabie, Mohammad Ali Youssofu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti ameyasema hayo Jumanne usiku katika kikao cha waandishi habari akiwa ameandamana na Ahmad Abul Gheit, Katibu Mkuu wa nchi za Kiarabu mjini Cairo.

Amesema Waarani wanapaswa kuwajibika kuhusu matatizo yaliyozikumba nchi zao na wachukue hatua za kutatua kadhia ya Syria.

Viongozi wa nchi za Kiarabu

Aidha amesema ukosefu wa umoja wa kisiasa na kiusalama katika nchi za Kiarabu, ni jambo ambalo limepelekea madola ya kigeni kuingilia mambo ya nchi hizo na hilo limepelekea zidhoofike na usalama wao kuvurigika zaidi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti amesema, nchi za Magharibi zimepelekea umoja wa nchi za Kiarabu kuvurugika.

Mgogoro wa Syria ulianza Machi mwaka 2011 ambapo magaidi na wanamgambo wanaopata uungaji mkono wa kigeni wamekuwa wakiendesha kampeni ya kikatili ya kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Assad. Syria inazilaumu nchi za Magharibi na waitifaki wao katika eneo hili kuwa ndio waungaji mkono wakubwa wa ugaidi nchini humo.