Makaburi 4 ya umati yagunduliwa Benghazi, Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i35121-makaburi_4_ya_umati_yagunduliwa_benghazi_libya
Maafisa wa polisi ya mji wa Benghazi huko kaskazini mwa Libya wamegundua makaburi manne ya umati katika eneo la kale la mji huo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 02, 2017 02:59 UTC
  • Makaburi 4 ya umati yagunduliwa Benghazi, Libya

Maafisa wa polisi ya mji wa Benghazi huko kaskazini mwa Libya wamegundua makaburi manne ya umati katika eneo la kale la mji huo.

Taarifa iliyotolewa na maafisa wa polisi wa Benghazi imesema kuwa, askari wa kitengo cha uchunguzi wa umma wamegundua makaburi manne ya umati yenye maiti za watu karibu 80 wasiojulikana katika eneo la Qanfuda huko kaskazini mwa Benghazi. 

Taarifa hiyo imeashiria harakati za kundi la kigaidi linalojiita Ansaru al Shari'a katika eneo hilo la kusema kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwamba, kundi hilo ndilo linalohusika na makaburi hayo.

Mwanasheria Mkuu wa Benghazi ametuma timu ya madaktari na maafisa wa jumuiya ya Hilali Nyekundu katika eneo hilo kwa ajili ya kuchunguza maiti hizo na kubaini sababu ya vifo vya watu hao.

Mwaka jana pia polisi ya Libya iligundua kaburi la umati katika eneo hilo hilo ambalo lilikuwa na maiti za watu 72.

Vita vya ndani Libya

Libya ilitumbukia katika vita na mapigano ya ndani baada na makundi ya nchi hiyo yakisaidiwa na Marekani na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kumuondoa madarakani kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi.