Waeritrea waandamana dhidi ya serikali kutokana na ukandamizaji wake kwa Waislamu
(last modified Wed, 01 Nov 2017 16:15:47 GMT )
Nov 01, 2017 16:15 UTC
  • Waeritrea waandamana dhidi ya serikali kutokana na ukandamizaji wake kwa Waislamu

Habari kutoka Eritrea zinaarifu kwamba raia wa nchi hiyo wamefanya maandamano makubwa kulaani hatua ya serikali ya Asmara katika kuwakandamiza Waislamu.

Kwa mujibu wa habari, maandamano hayo yalifanyika jana katika eneo la Akriya la mji wa Asmara, ambao ni mji mkuu wa Eritrea katka kulalamikia hatua za serikali kuwalenga Waislamu. Hii ni baada ya polisi kuwatia mbaroni viongozi wengi wa shule za Kiislamu katika eneo hilo na kwenda nao kusikojulikana.

Maandamano ya Waislamu mjini Asmara

Kwa mujibu wa habari, serikali imewatia mbaroni viongozi hao wa shule za Kiislamu baada ya wao kupinga amri ya serikali ya kutaka kubadili mitaala ya masomo ya dini yao sambamba na kupiga marufuku vazi la hijabu kwa wanafunzi wa kike. Aidha serikali ya Asmara imepiga marufuku masomo ya dini katika shule za mji huo wenye Waislamu wengi, suala ambalo limezusha hasira kali kwa raia wa Eritrea. Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti risasi zimesikika katika maandamano hayo baada ya polisi kujaribu kuwatawanya waandamanaji.

Tags