Macron: Ni wakati wa kusonga mbele na kusahau zama za kukoloniwa Algeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i37275-macron_ni_wakati_wa_kusonga_mbele_na_kusahau_zama_za_kukoloniwa_algeria
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa yuko Algeria katika ziara ya siku moja ambapo amesisitiza suala la kufunguliwa ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi mbili hizio na kusema kuwa, hatoendelea kuwa mateka wa zama zilizopita za ukoloni wa Ufaransa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 06, 2017 22:06 UTC
  • Macron: Ni wakati wa kusonga mbele na kusahau zama za kukoloniwa Algeria

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa yuko Algeria katika ziara ya siku moja ambapo amesisitiza suala la kufunguliwa ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi mbili hizio na kusema kuwa, hatoendelea kuwa mateka wa zama zilizopita za ukoloni wa Ufaransa.

Rais wa Ufaransa yupo Algiers mji mkuu wa Algeria kwa ajili ya mazungumzo na Rais Abdelaziz Bouteflika wa nchi hiyo na maafisa wa ngazi ya juu, huku wakati huo huo akijaribu kuimarisha mahusiano ya kijamii na kibiashara  kati ya nchi mbili.

Uhusiano wa Ufaransa na Algeria ni uhusiano ulioathiriwa na majeraha ya vita vya kupigania uhuru kuanzia mwaka 1954 hadi 1962; ambapo mamia ya maelfu ya wananchi wa Algeria waliuawa na mateso kushuhudiwa baina ya pande zote mbili.

Wahanga wa vita vya ukombozi wa Algeria kuanzia mwaka 1954-1962 

Rais Bouteflika wa Algeria aliye na umri wa miaka 80 ni miongoni mwa wakongwe wa kivita waliopigana dhidi ya ukoloni wa Ufaransa na afya yake imekuwa ikidhoofika tangu apatwe na maradhi ya kupooza mwaka 2013. Akihojiwa na gazeti la Al Watan la nchini Algeria, Rais wa Ufaransa amesema kuwa na hapa ninamnukuu" nafahamu historia, hata hivyo mimi si mateka wa zama zilizopita. Tuna kumbukumbu za pamoja na tunahitaji kukubali hilo, lakini ninataka mbali na kuheshimu historia yetu, tuangalie mustakbali ulioko mbele yetu," mwisho wa kunukuu.