Rais wa Somalia amfuta kazi meya wa Mogadishu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i39277-rais_wa_somalia_amfuta_kazi_meya_wa_mogadishu
Rais wa Somalia Mohammad Abdullahi leo amemfuta kazi meya wa mji mkuu Mogadishu na kumteua waziri wa habari kuchukua nafasi yake.
(last modified 2026-04-28T05:09:17+00:00 )
Jan 21, 2018 10:37 UTC
  • Rais wa Somalia amfuta kazi meya wa Mogadishu

Rais wa Somalia Mohammad Abdullahi leo amemfuta kazi meya wa mji mkuu Mogadishu na kumteua waziri wa habari kuchukua nafasi yake.

Katika taarifa, Rais Abdullahi amemteua Abdirahman Omar Osman kama meya mpya baada ya kumuondoa Taabit Abdi Mohamed. Ofisi ya Rais haikutangaza sababu ya kufutwa kazi Mohammad.

Kumekuwa na tetesi katika vyombo vya habari vya ndani ya Somalia kuwa Mohammad alikuwa hasikilizani na Waziri Mkuu Hassan Khaire.

Wakaazi wa Mogadishu wanasema maafisa wa usalama Jumamosi usiku waliingia katika ofisi ya meya huku barabra muhimu za mji wa Mogadishu zikiwa zimefungwa leo Jumapili.

Waziri wa habari aliyeteuliwa kuwa meya hajazungumza na waandishi habari kuhusu uteuzi huo.

Image Caption

Somalia ilitumbukia katika mapigano ya ndani mwaka 1991 wakati dikteta wa muda mrefu wa nchi hiyo, Mohammad Siad Barre alipopinduliwa.

Serikali ya Somalia ambayo sasa inaungwa mkono na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika, AMISOM imekuwa ikijitahidi kuwaangamiza magaidi wa al Shabab. Ingawa magaidi hao wamedhoofika sana lakini hutekeleza hujuma za kuvizia mara kwa mara nchini Somalia hasa katika mji mkuu Mogadishu na pia katika nchi jirani ya Kenya.