Watu 15 wauawa katika wimbi jipya la machafuko Kasai, DRC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i40969-watu_15_wauawa_katika_wimbi_jipya_la_machafuko_kasai_drc
Watu wasiopungua 15 wameuawa katika wimbi jipya la mapigano katika eneo la Kasai huko Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 28, 2018 04:25 UTC
  • Watu 15 wauawa katika wimbi jipya la machafuko Kasai, DRC

Watu wasiopungua 15 wameuawa katika wimbi jipya la mapigano katika eneo la Kasai huko Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo.

Andre Kapiola, chifu wa eneo la Lombelu mkoani Kasai amesema askari mmoja wa serikali na wapiganaji 14 wa kundi la waasi wa Kamwina Nsapu wameuawa katika mapigano hayo mapya.

Mkoa wa Kasai umekuwa uwanja wa makabiliano kati ya jeshi la serikali na waasi wa Kamwina Nsapu, kiongozi wa kikabila aliyeuawa na maafisa usalama mnamo Septemba mwaka 2016.

Kundi la Kamwina Nsapu lilianzisha harakati hizo kupinga hatua ya Rais Joseph Kabila kuendelea kung'ang'ania madaraka licha ya muhula wake kisheria kumalizika. 

Ramani ya DRC inayoonyesha mkoa wa Kasai

Haya yanajiri katika hali ambayo, watu watu 22 waliuawa baada ya kundi la waasi wa Nyatura ambao aghalabu yao wanatoka kabila la Wahutu kuvamia vijiji vya Kalusi na Bwalanda na kukabiliana na waasi wa genge la Mai Mai Mazembe siku ya Jumapili na Jumatatu iliyopita.

Maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yanashuhudia machafuko na mapigano kwa zaidi ya miaka 20 sasa.