Makumi wapoteza maisha kwa ugonjwa wa uti wa mgongo Niger
(last modified Sun, 03 Apr 2016 02:21:21 GMT )
Apr 03, 2016 02:21 UTC
  • Makumi wapoteza maisha kwa ugonjwa wa uti wa mgongo Niger

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, makumi ya watu wamepoteza maisha nchini Niger kutokana na ugonjwa wa uti wa mgongo.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, ripoti mpya iliyotolewa kati ya mwezi Januari na mwezi Machi mwaka huu, inaonyesha kwamba watu 61 kati ya watu 730 waliokumbwa na ugonjwa huo wa uti wa mgongo, wamepoteza maisha nchini humo. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya wahanga wa maradhi hayo ni watoto na vijana walio kati ya umri wa miaka 5 hadi 14. Aidha ripoti hiyo imeeleza kuwa, mwaka uliopita zaidi ya watu 573 walipoteza maisha ndani ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Ofisi ya uratibu katika masuala ya kibinaadamu iliyo chini ya Umoja wa Mataifa imetangaza mahitaji ya dozi ya chanjo milioni tatu na laki mbili za kuzuia mambukizi ya homa hiyo nchini Niger. Inaelezwa kuwa, hatari ya ugonjwa huo inahisika sana katika maeneo yaliyoshuhudia maradhi hayo mwaka uliopita.

Tags