Idadi ya watu waliopoteza maisha katika hujuma mbili Nigeria yaongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46062-idadi_ya_watu_waliopoteza_maisha_katika_hujuma_mbili_nigeria_yaongezeka
Idadi ya wahanga wa miripuko miwili ya kujitoa muhanga kaskazini mashariki mwa Nigeria imeongezeka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 19, 2018 09:21 UTC
  • Idadi ya watu waliopoteza maisha katika hujuma mbili Nigeria yaongezeka

Idadi ya wahanga wa miripuko miwili ya kujitoa muhanga kaskazini mashariki mwa Nigeria imeongezeka.

Viongozi wa serikali ya Nigeria wamesema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha katika hujuma za kujitoa muhanga katika mji wa Damboa, jimbo la Borno imefikia 43. Awali vyanzo vya habari mjini Damboa vilitangaza kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha katika miripuko miwili iliyotokea siku ya Jumapili iliyopita imefikia 31 na wengine kujeruhiwa. Kwa mujibu wa viongozi wa mji huo, hujuma hizo zilitekelezwa na wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram.

Magaidi wa kundi la Boko Haram

Kundi hilo la kigaidi lilianzisha shughuli zake tangu mwaka 2009 katika nchi za eneo la Ziwa Chad zikiwemo, Nigeria, Niger na Cameroon. Hadi sasa operesheni za kigaidi za wanachama wa kundi hilo hatari lenye kufuata idolojia ya Uwahabi, zimesababisha watu elfu 20 kuuawa na wengine zaidi ya milioni mbili na laki sita kuwa wakimbizi.