Watu 25 waaga dunia kwa maradhi ya kipindupindu Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46192-watu_25_waaga_dunia_kwa_maradhi_ya_kipindupindu_nigeria
Watu wasiopungua 25 wamefariki dunia kaskazini mashariki mwa Nigeria kufuatia maradhi ya kipindupindu yaliyoibuka katika maeneo hayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 22, 2018 09:40 UTC
  • Watu 25 waaga dunia kwa maradhi ya kipindupindu Nigeria

Watu wasiopungua 25 wamefariki dunia kaskazini mashariki mwa Nigeria kufuatia maradhi ya kipindupindu yaliyoibuka katika maeneo hayo.

Serikali ya Nigeria imetangaza kupitia taarifa yake rasmi kwamba, kesi nyingine mpya 12 za maradhi ya kipindupindu zimeripotiwa  kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na kwamba, idadi ya watu walioambukizwa maradhi hayo imefikia 349.

Aidha taarifa hiyo ya serikkali ya Nigeria imeeleza kuwa, tangu mwezi uliopita wa Mei hadi sasa majimbo kadhaa ya nchi hiyo yakiwemo ya Adamawa la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo yamekumbwa na maradhi ya kipindupindu.

Ugonjwa huo wa kipindupindu ambao awali ulilipuka katika maeneo ya watu maskini na yenye idadi kubwa ya watu kaskazini mashariki mwa Nigeria, baadaye ulienea katika maeneo mengine. 

Wanamgambo wa Boko Haram

Wataalamu wa afya nchini Nigeeria wanasema kuwa, ugonjwa wa kipindupindu umekuwa ukiibuka katika maeneo mengi ya nchi hiyo yenye wakazi wengi na ambayo yana mfumo duni wa kudhamini maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu.

Itakumbukwa kuwa, maeneo hayo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria yamekuwa yakishuhudia pia mauaji makubwa kutokana na kuwa ngome kuu ya wanamgambo wa kuundi la kigaidi la Boko Haram.

Tokea kundi la kigaidi la Boko Haram lianzishe uasi wake nchini Nigeria mwaka 2009, watu zaidi ya 20 elfu wameuawa, huku wengine zaidi ya milioni mbili wakilazimika kuwa wakimbizi kutokana na ugaidi wa kundi hilo.