Zaidi ya watu 80 wameuawa katika mapigano ya kikabila nchini Nigeria
Polisi nchini Nigeria imetangaza habari ya kuuawa watu 86 katika mapigano mapya ya kikabila yaliyotokea katikati ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Polisi ya Nigeria imetangaza habari hiyo leo na kuongeza kuwa, watu hao 86 wameuawa katika mapigano yaliyotokea siku za hivi karibuni kwenye jimbo la Plateau la katikati mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa jeshi hilo la polisi, mapigano hayo yamezuka baina ya wakulima na wafugaji ambao si wakazi wa eneo hilo.
Serikali ya Nigeria imetangaza hali ya hatari na kupiga marufuku watu kutoka nje katika jimbo hilo la Plateau kuanzia saa 12 jioni hadi 12 asubuhi kama ambavyo imetangaza serikali ya kijeshi katika eneo hilo katika juhudi zake za kujaribu kurejesha utulivu na hali ya kawaida.
Mapigano ya kikabila nchini Nigeria yanatokea mbali sana, yamekuwepo kwa makumi ya miaka sasa ingawa yameongezeka zaidi katika miezi ya hivi karibuni.
Mbali na chuki na uhasama wa kikabila, tatizo jingine kubwa la Nigeria ni ongezeko la uuzaji wa silaha kinyume cha sheria ambao hivi sasa umeripoti kuongezeka na hivyo kuzidisha hali mbaya ya kiusalama, ukatili na machafuko katika nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.
Tatizo jingine kubwa ni wanamgambo wa genge la kigaidi la Boko Haram ambao mashambulizi yao hadi hivi sasa yameshasababisha mauaji ya watu waziopungua 20 elfu 20 huko kaskazini mashariki mwa Nigeria na wamekuwa wakiingiza silaha nchini humo kwa njia za magendo kupitia kaskazini mwa Afrika hususan nchini Libya.