UN Yapongeza Ziara ya Kihistoria ya Ujumbe wa Eritrea nchini Ethiopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46427-un_yapongeza_ziara_ya_kihistoria_ya_ujumbe_wa_eritrea_nchini_ethiopia
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza ziara iliyofanywa na ujumbe wa ngazi wa juu wa Eritrea nchini Ethiopia, ikiwa ni hatua ya kwanza inayolenga kuurejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili uwe wa kawaida.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 29, 2018 00:00 UTC
  • UN Yapongeza Ziara ya Kihistoria ya Ujumbe wa Eritrea nchini Ethiopia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza ziara iliyofanywa na ujumbe wa ngazi wa juu wa Eritrea nchini Ethiopia, ikiwa ni hatua ya kwanza inayolenga kuurejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili uwe wa kawaida.

Guterres amesema kupitia kwa msemaji wake Stephane Dujarric, kuwa hatua hiyo ya kidiplomasia ya kupunguza taharuki na kutatua mgogoro wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili, itatoa athari chanya kwa kanda nzima. Amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kuunga mkono nchi hizo mbili kutekeleza uamuzi kuhusu mpaka au katika eneo lingine ambalo zinaona ni muhimu kwa Umoja huo kutoa msaada.

Ujumbe wa Eritrea ulioongozwa na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Osman Saleh uliwasili Addis Ababa Jumanne kwa ziara ya kihistoria, ambayo ni ya kwanza kufanyika katika miongo miwili.

Ethiopia na Eritrea zilipigana kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2000, na kusababisha vifo vya watu elfu 80 kutokana na mgogoro wa mpaka.