Afya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky yazidi kuwa mbaya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46703-afya_ya_sheikh_ibrahim_zakzaky_yazidi_kuwa_mbaya
Habari kutoka kwa watu walio karibu na familia ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ambaye anaendelea kushikiliwa na vyombo vya uusalama vya nchi hiyo zinasema kuwa, hali ya kiafya ya mwanaharakati huyo wa Kiislamu imezidi kuwa mbaya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 11, 2018 03:15 UTC
  • Afya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky yazidi kuwa mbaya

Habari kutoka kwa watu walio karibu na familia ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ambaye anaendelea kushikiliwa na vyombo vya uusalama vya nchi hiyo zinasema kuwa, hali ya kiafya ya mwanaharakati huyo wa Kiislamu imezidi kuwa mbaya.

Yunus Abubakar mwandishi wa habari na mtuu wa karibu na familia ya Sheikh Ibrahim Zakzaky ametoa wito wa kuachiliwa huru mwanaharakati huyo mashuhuri wa Kiislamu. Yunus ameeleza kuuwa, hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky aliyeko korokoroni inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.

Wakati huo huo, Ibrahim Mussa, Msemaji wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria  amesisitiza juu ya udharura wa kuweko uangalizi wa kitiba kwa Sheikh Zakzaky na kuitaka serikali ya Nigeria imuachilie huru haraka kiongozi huyo wa Kiislamu ili aweze kupatiwa matibabu.

Wakati huo huo, maandamano ya kushinikiza kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky yameendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ya Nigeria huku serikali ya nchi hiyo ikiendelea kukaidi amri ya mahakama ya kumuachilia huru mwanaharakati huyo wa Kiislamu.

Maandamano ya kuishinikiza serikali ya Nigeria imuachilie huru Sheikh Ibrahim Zakzaky

Ikumbukwe kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky, mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alikamtwa baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya yeye na mke wake mwezi Disemba 2015 wakati jeshi la nchi hiyo lilipovamia Husainia ya Baqiyyatullah mjini Zaria na kuua kwa umati mamia ya Waislamu.

Hivi sasa miaka miwili na nusu imepita tangu kutokea uvamizi huo lakini serikali ya Nigeria ingali inang'ang'ania kumshikilia korokoroni Sheikh Ibrahim Zakzaky licha ya kuwa mwaka 2016 Mahakama Kuu ya nchi hiyo ilitoa amri ya kuachiliwa huru.