UN yaitaka Sudan Kusini kupambana haraka na uvunjaji wa haki za watoto
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47982-un_yaitaka_sudan_kusini_kupambana_haraka_na_uvunjaji_wa_haki_za_watoto
Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya watoto na mapigano ya kutumia silaha ameisisitizia serikali ya Sudan Kusini wajibu wake wa kuchukua hatua za haraka za kupambana na uvunjaji wa haki za watoto na kuwapandisha kizimbani wahalifu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 08, 2018 10:21 UTC
  • UN yaitaka Sudan Kusini kupambana haraka na uvunjaji wa haki za watoto

Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya watoto na mapigano ya kutumia silaha ameisisitizia serikali ya Sudan Kusini wajibu wake wa kuchukua hatua za haraka za kupambana na uvunjaji wa haki za watoto na kuwapandisha kizimbani wahalifu.

Virginia Gamba, mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya watoto na vita vya kutumia silaha amesema kuwa, kumetokea uvunjaji mkubwa wa haki za watoto huko Sudan Kusini na jambo hilo halikubaliki kabisa, hivyo kuna wajibu wa kuchukuliwa hatua za haraka za kulindwa haki za watoto hao na kukomeshwa kikamilifu vitendo hivyo viovu.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, mwaka 2017 karibu watoto 400 wa Sudan Kusini walikuwa wahanga wa moja kwa moja wa machafuko ya nchi hiyo.

 

Kuna maelefu ya wasichana na wavulana nao wamepata hasara kubwa kutokana na mapigano ya kutumia silaha nchini Sudan Kusini.

Hadi hivi sasa vita vya ndani vya Sudan Kusini vimeshapelekea makumi ya maelfu ya watu kuuawa na milioni nne wengine kuwa wakimbizi.

Mwaka 2011 na kwa uchochezi wa nchi za Magharibi hasa Marekani, eneo la Sudan Kusini lilijitenga na ndugu zake wa Sudan. Hata hivyo tangu wakati huo nchi hiyo changa zaidi barani Afrika haijawahi kuwa na utulivu wa kudumu. Machafuko yalishadidi nchini humo mwezi Disemba 2013 baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu makamu wake wakati huo, Riek Machar kwamba alikuwa na nia ya kumpindua.