Jeshi la Nigeria lazima shambulizi la magaidi wa Boko Haram
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48120-jeshi_la_nigeria_lazima_shambulizi_la_magaidi_wa_boko_haram
Duru za kijeshi za Nigeria zimetangaza kuwa, kundi la kigaidi la Boko Haram limeshambulia kambi nyingine ya kijeshi kaskazini mwa nchi hiyo lakini shambulio hilo limezimwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 13, 2018 22:51 UTC
  • Jeshi la Nigeria lazima shambulizi la magaidi wa Boko Haram

Duru za kijeshi za Nigeria zimetangaza kuwa, kundi la kigaidi la Boko Haram limeshambulia kambi nyingine ya kijeshi kaskazini mwa nchi hiyo lakini shambulio hilo limezimwa.

Duru za kijeshi za Nigeria katika mji wa Maiduguri ambao ni makao makuu ya jimbo la Borno la kaskazini mashariki mwa Nigeria zimetangaza kuwa, hatimaye jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuzima shambulizi la magaidi wa Boko Haram katika kambi ya kijeshi ya mji wa Damasak mkoani humo baada ya masaa kadhaa ya mapigano.

Duru hizo zimeongeza kuwa, makumi ya magaidi wa Boko Haram Jumatano usiku walivamia kambi ya kijeshi ya Damasak kwa nia ya kuiteka.

Alkhamisi ya tarehe 6 Septemba pia magaidi wa Boko Haram walishambulia kambi moja ya jeshi la Nigeria katika jimbo hilo la Borno na mbali na kuiteka kambi hiyo, waliua pia wanajeshi wasiopungua 48 wa serikali.

Kundi hilo la kigaidi lilianzishwa mwaka 2009 kaskazini mwa Nigeria na hadi hivi sasa limeshaua zaidi ya watu 20 elfu nchini Nigeria na katika nchi jirani na limeshapelekea zaidi ya watu milioni mbili na laki sita kuwa wakimbizi.