Kipindupindu chaua watu 97 kaskazini mwa Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48324-kipindupindu_chaua_watu_97_kaskazini_mwa_nigeria
Watu wasiopungua 97 wamefariki dunia kaskazini mashariki mwa Nigeria kufuatia mripuko wa maradhi ya kipindupindu katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 22, 2018 23:58 UTC
  • Kipindupindu chaua watu 97 kaskazini mwa Nigeria

Watu wasiopungua 97 wamefariki dunia kaskazini mashariki mwa Nigeria kufuatia mripuko wa maradhi ya kipindupindu katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imetangaza kwamba, kesi za ugonjwa huo zilizorekodiwa kufikia sasa katika majimbo ya Yobe na Borno ni 3,126, vikiwemo vifo 97.

Mripuko wa maradhi hayo hatarishi ulitangazwa wiki mbili zilizopita jimboni Borno, ambako mamia ya maelfu ya wakimbizi wa ndani wanaishi kambini, baada ya kuyahama makazi yao wakihofia mashambuizi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.

 

Usafi, nguzo muhimu ya kupambana na kipindupindu

Haya yanajiri siku chache baada ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini Nigeria kuua watu zaidi ya 100 katika majimbo 10 ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Nigeria iliyoko magharibi mwa bara la Afrika ni miongoni mwa nchi ambazo hukumbwa na mafuriko karibu kila mwaka ambapo mvua kubwa hunyesha nchini humo baina ya mwezi Mei na Septemba.