Wanajeshi wanne wa Misri wauawa mapiganoni katika mkoa wa Sinai
Wanajeshi wanne wa Misri wameuawa katika mapigano kati ya jeshi la serikali na makundi ya waasi katika mkoa wa Sinai ya kaskazini nchini humo.
Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imetangaza kuwa, wanajeshi wengine watano wa Misri wamejeruhiwa katika mapigano hayo yaliyojiri mashariki mwa eneo la Al Arish na magharibi mwa mji wa Rafah katika mkoa wa Sinai ya kaskazini. Mapigano kati ya askari usalama wa Misri na watu wenye silaha yamepamba moto katika mkoa wa Sinai ya Kaskazini tangu Rais Abdel Fattah al Sisi aliposhika madaraka ya nchi mwaka 2014.
Kundi la kigaidi katika eneo la Sinai ambalo ni tawi la kijeshi la kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh hadi sasa limefanya mashambulizi kadhaa ya kigaidi dhidi ya jeshi na polisi ya Misri na kuuwa na kujeruhi makumi ya askari hao.