Tume ya uchaguzi Kongo yaakhirisha uchaguzi katika miji mitatu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50438-tume_ya_uchaguzi_kongo_yaakhirisha_uchaguzi_katika_miji_mitatu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo imesema kuwa imeakhirisha katika miji mitatu nchini humo uchaguzi wa rais na wa bunge uliopangwa kufanyika Jumapili ya tarehe 30 mwezi huu hadi mwezi ujao wa Machi.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Dec 26, 2018 11:12 UTC
  • Tume ya uchaguzi Kongo yaakhirisha uchaguzi katika miji mitatu

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo imesema kuwa imeakhirisha katika miji mitatu nchini humo uchaguzi wa rais na wa bunge uliopangwa kufanyika Jumapili ya tarehe 30 mwezi huu hadi mwezi ujao wa Machi.

Hatua hii inamaanisha kuwa kura za miji hiyo mitatu hazitajumuishwa katika mchuanao wa kiti cha urais.  

Miji hiyo mitatu huko Kongo ambayo uchaguzi umeakhirishwa ni Beni na Butembo inayopatikana mashariki mwa nchi hiyo ambayo imekuwa ikisumbuliwa na homa ya Ebola tangu mwezi Agosti ; na pia mji wa Yumbi magharibi mwa nchi ambako watu zaidi ya 100 waliuawa wiki iliyopita katika machafuko ya kikabila. 

Uchaguzi waakhirishwa Beni na Butembo kutoka na maradhi ya Ebola 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongeza kuwa chaguzi hizo mbili zitafanyika kama ilivyopangwa siku ya Jumapili. Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais yatatangazwa Januari 15 mwaka 2019 na Rais mpya ataapishwa Januari 18. Itakumbukwa kuwa uchaguzi wa rais na bunge ulipangwa kufanyika tarehe 23 Disemba hata hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo iliuakhirisha kutokana na mkasa wa moto uliotokea ambao uliteketeza vifaa vya uchaguzi kwa ajli ya mji mkuu Kinshasa.