Magaidi 16 wauawa Sinai Kaskazini nchini Misri
(last modified Tue, 19 Feb 2019 15:42:44 GMT )
Feb 19, 2019 15:42 UTC
  • Magaidi 16 wauawa Sinai Kaskazini nchini Misri

Jeshi la Misri limewauwa magaidi 16 katika oparesheni ya ulipizaji kisasi iliyoifanya katika mji wa Arisha katika eneo la Sinai Kaskazini.

Shirika la habari la serikali la Al Ahram limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, operesheni mbili za kulipiza kisasi zimefanyika katika wilaya za Obeidat na Abu Eita katika mji huo wa Arish, ambapo magaidi 16 wameangamizwa.

Aidha kiasi ambacho hakijatajwa cha silaha kama vile bunduki, risasi na mada za miripuko kimepatika katika operesheni iliyofanyika katika wilaya ya Abu Eita. 

Hapo jana, askari watatu wa jeshi la Misri waliuawa katika mripuko wa bomu huko Sinai Kaskazini, huku wengine sita wakijeruhiwa. 

Wanajeshi wa Misri katika Peninsula ya Sinai

Aidha Jumamosi iliyopita, wanamgambo saba waliuawa katika makabiliano na jeshi la Misri katika eneo hilo Sinai, ambapo iliripotiwa pia kuwa wanajeshi 15 wa Misri waliuawa au kujeruhiwa.

Mapigano kati ya askari usalama wa Misri na watu wenye silaha katika mkoa huo wa Sinai Kaskazini ambayo yameua makumi ya raia na maafisa usalama yalishika kasi mwaka 2014 baada ya Rais Abdul Fattah al Sisi kushika madaraka ya nchi hiyo. 

Tags