Guterres ataka kupunguzwa wanajeshi 2000 wa Monusco waliopo Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i52075-guterres_ataka_kupunguzwa_wanajeshi_2000_wa_monusco_waliopo_kongo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kupunguzwa wanajeshi elfu mbili wa kikosi cha kulinda amani cha umoja huo waliopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Monusco).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 10, 2019 10:32 UTC
  • Guterres ataka kupunguzwa wanajeshi 2000 wa Monusco waliopo Kongo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kupunguzwa wanajeshi elfu mbili wa kikosi cha kulinda amani cha umoja huo waliopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Monusco).

Antonio Guterres amewasilisha ripoti kwa Baraza la Usalama na kupendekeza kupunguzwa wanajeshi  elfu mbili waliopo katika kikosi cha kulinda amani cha UN waliopo Kongo (Monusco). Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa ametoa pendekezo la kupunguzwa idadi hiyo ya wanajeshi kutokana na kupungua vyanzo vya fedha vya Umoja wa Mataifa. 

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa UN
 

Umoja wa Mataifa hivi sasa unakabiliwa na matatizo ya kifedha kwa sababu Marekani imepunguza kiwango cha mchango wake wa fedha kwa ajili ya kudhamini bajeti ya umoja huo; huku nchi nyingi kadhaa pia zikiwa bado hazijatoa mchango wao kwa Umoja wa Mataifa. Pendekezo hilo la Guterres la kupunguzwa wanajeshi walinda amani huko Kongo linatazamiwa kuchunguzwa kabla ya kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili suala la kuongeza muda wa kuhudumu kikosi cha Monusco huko Kongo. Umoja wa Mataifa umekuwa ukitekeleza majukumu ya kulinda amani huko Kongo yapata miaka ishirini sasa.