Umoja wa Afrika wasisitiza ulazima wa kufanyika mazungumzo ya kitaifa Algeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i52224-umoja_wa_afrika_wasisitiza_ulazima_wa_kufanyika_mazungumzo_ya_kitaifa_algeria
Umoja wa Afrika (AU) umesisitiza kwamba kuna ulazima wa kufanyika mazungumzo ya kitaifa nchini Algeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 17, 2019 13:33 UTC
  • Umoja wa Afrika wasisitiza ulazima wa kufanyika mazungumzo ya kitaifa Algeria

Umoja wa Afrika (AU) umesisitiza kwamba kuna ulazima wa kufanyika mazungumzo ya kitaifa nchini Algeria.

Umoja huo umetaka kufanyike mazungumzo ya kitaifa nchini Algeria ili kuandaa mazingira mazuri ya kutekelezwa kile kilichotajwa kuwa ni mapendekezo ya marekebisho ya  Rais wa nchi hiyo, Abdelaziz Bouteflika. Maandamano makuwba ya wananchi wa Algeria yanayoendelea hadi sasa tangu mwezi mmoja uliopita yamemlazimisha Rais wa nchi hiyo kutupilia mbali uamuzi wake wa kugombea kiti cha rais kwa muhula wa tano. Hata hivyo kiongozi huyo ameamua kuakhirisha uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi ujao wa Aprili, suala ambalo limepingwa vikali na makundi ya kisiasa na matabaka mbalimbali ya ya wananchi. 

Rais Boutefika wa Algeria

Abdelaziz Bouteflika ameshirika katika chaguzi zote za rais tangu mwanzoni mwaka 1999 na kuendelea kusalia madarakani kutokana na uungaji mkono wa muungano wa chama tawala.

Bouteflika alitangaza  kuachana na uamuzi wake wa kugombea kiti cha urais siku tano silizopita  na kusema kuwa, uchaguzi huo uliotazamiwa kufanyika mwezi ujao wa Aprili utasogezwa mbele kidogo kwa ajili ya kutoa fursa ya kufanyika Kongamano la Kitaifa kuhusu mustakabali wa kisiasa nchini humo.

Waalgeria wamekuwa wakifanya maandamano kumshinikiza Rais huyo kung'atuka madarakani kutokana utendaji wake dhaifu. Vilevile hali ya kiafya ya Abdelaziz Bouteflika imekuwa ikizorota siku baada ya siku kutokana na maradhi ya muda mrefu.