Waziri Mkuu wa Algeria aanza mazungumzo ya kuunda serikali mpya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i52234-waziri_mkuu_wa_algeria_aanza_mazungumzo_ya_kuunda_serikali_mpya
Waziri Mkuu wa Algeria ameanza mazungumzo ya kuunda serikali mpya kama hatua iliyochukuliwa ili kuwaridhisha wananchi wanaofanya maandamanao wakiomtaka Rais wa nchi hiyo, Abdelaziz Bouteflika na serikali yake wang'atuke madarakani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 17, 2019 21:56 UTC
  • Waziri Mkuu wa Algeria aanza mazungumzo ya kuunda serikali mpya

Waziri Mkuu wa Algeria ameanza mazungumzo ya kuunda serikali mpya kama hatua iliyochukuliwa ili kuwaridhisha wananchi wanaofanya maandamanao wakiomtaka Rais wa nchi hiyo, Abdelaziz Bouteflika na serikali yake wang'atuke madarakani.

Taarifa za duru rasmi za Algeria zinasema kuwa serikali hiyo mpya itawajumuisha wataalamu na itaakisi idadi ya jamii ya Algeria.

Kuna uwezekano pia kwamba Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo Noureddine Bedoui atafanikiwa kupunguza kiwango cha hasira za wananchi wanaofanya maandamano kwa kuanzisha mazungumzo hayo ya kuunda serikali mpya.

Hivi karibuni Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria hatimaye alitupilia mbali uamuzi wake wa awali wa kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tano na kusema ataendelea kuwepo madarakani hadi katiba mpya itakapoandaliwa. Weledi wa kisiasa wameitaja hatua hiyo ya Bouteflika kuwa ni sawa na kujiongezea muda wa kuweko madarakani.

Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria

Hata hivyo wafanya maandamano nchini humo wameweka wazi kwamba wanataka kuona nchi yao inakuwa na uongozi wa kizazi kipya.