Jeshi la Algeria lasisitiza kuyapatia ufumbuzi matatizo na kuwaunga mkono wananchi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i52261-jeshi_la_algeria_lasisitiza_kuyapatia_ufumbuzi_matatizo_na_kuwaunga_mkono_wananchi
Mkuu wa vikosi vya jeshi la Algeria amesisitiza kuwa vikosi vya nchi hiyo vitaendelea kuwa pamoja na wananchi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 19, 2019 03:35 UTC
  • Jeshi la Algeria lasisitiza kuyapatia ufumbuzi matatizo na kuwaunga mkono wananchi

Mkuu wa vikosi vya jeshi la Algeria amesisitiza kuwa vikosi vya nchi hiyo vitaendelea kuwa pamoja na wananchi.

Ahmad Qaid Saleh amesisitiza kuwa kuna njia ya amani ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo na kueleza kuwa: Jeshi la Algeria siku zote limekuwa bega kwa bega na wananchi.

Mkuu wa vikosi vya jeshi la Algeria amebainisha kuwa jeshi la nchi hiyo lina imani kuwa wananchi wana uwezo wa kutosha ili kuzizuia nchi ajinabi kutumia vibaya hali ya kisiasa ya nchi hiyo.  

Maeneo mbalimbali ya Algeria yanaendelea kukumbwa na maandamano ya wananchi licha ya Rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika kutangaza kuachama na uamuzi wake wa kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tano sambamba na kuakhirishwa tarehe ya uchaguzi huo. Wafanya maandamano wanamtaka Bouteflika ang'atuke madarakani. 

Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria

Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria wiki iliyopita alitoa dikrii na Amri ya Rais kuakhirisha uchaguzi wa rais uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 18 mwezi Aprili mwaka huu baada ya kujiri maandamano nchini humo kwa wiki kadhaa sasa.

Hata hivyo wapinzani nchini Algeria wameitaja dikrii hiyo kuwa ni kinyume cha sheria na kumtuhumu Bouteflika kuwa anafanya kila anachoweza ili kuandaa mazingira ya kuimarisha misingi ya kusalia madarakani.