Kenya yatenga dola milioni 18.8 kukabiliana na njaa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i52769-kenya_yatenga_dola_milioni_18.8_kukabiliana_na_njaa
Kenya imetenga dola milioni 18.8 (Ksh Bilioni 1.88) kukabiliana na baa la njaa nchini humo ambaloo limewaathiri watu takriban milioni 1.1.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 11, 2019 01:46 UTC
  • Kenya yatenga dola milioni 18.8 kukabiliana na njaa

Kenya imetenga dola milioni 18.8 (Ksh Bilioni 1.88) kukabiliana na baa la njaa nchini humo ambaloo limewaathiri watu takriban milioni 1.1.

Waziri wa Ugatuzi Kenya Eugene Wamalwa amesema wataalamu wametabiri kuwa mvua haitanyesha kwa wakati na kwa msingi huo serikali imeandaa fedha kusaidia kukabiliana na janga hilo.

Wamalwa pia amesema, serikali imetoa dola milioni 6 kununua magunia elfu 26,200 ya mahindi, elfu 17,060 ya maharagwe na elfu 15,420 ya mchele ambavyo tayari vimeshatolewa kwa wahitaji, na dola nyingine milioni 6.8 zimepelekwa kwenye idara ya maji kwa ajili ya kusafirisha maji na kukarabati visima.

Serikali ya Kenya  imekanusha taarifa kwamba watu kadhaa wamekufa kutokana na njaa inayosababishwa na ukame ambao kwa sasa umeyaathiri maeno ya kaskazini magharibi mwa nchi .

Naibu Rais wa Kenya William Ruto

Waziri Wamalwa amesema kulikuwa na vifo , lakini akaongeza kuwa haviwezi kuhusishwa na ukame.

Naye Naibu rais wa Kenya William Ruto amesema Kenya iko na uwezo mzuri wa kukabiliana na ukame ikilinganishwa na miaka iliyopita huku akisisitiza kwamba watu hakuna Mkenya aliyepoteza maisha kutokana na njaa.

Kaunti za Turkana na Baringo ndizo zilizoathiriwa vibaya zaidi na baa la njaa.