Mamia watoweka baada ya boti kuzama magharibi mwa DRC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i53747-mamia_watoweka_baada_ya_boti_kuzama_magharibi_mwa_drc
Mamia ya watu hawajulikani waliko baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Mai-Ndombe magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 27, 2019 03:07 UTC
  • Mamia watoweka baada ya boti kuzama magharibi mwa DRC

Mamia ya watu hawajulikani waliko baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Mai-Ndombe magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maafisa wa serikali katika eneo hilo wamesema boti hiyo ilizama usiku wa kuamkia jana. Hakuna taarifa yoyote rasmi iliyotolewa na serikali ya DRC kuhusu maafa yaliyosababishwa na ajali hiyo.

Hata hivyo mashuhuda wanasema makumi ya watu wamenusurika katika ajali hiyo na kwamba hatima ya wengine 200 haijulikani.

Mwezi uliopita, watu 37 walifariki dunia baada ya boti yao kuzama katika Ziwa Kivu katika mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ramani ya Kongo DR

Ajali za boti zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara DRC, na sababu kuu ya ajali hizo ni boti kujaza watu kupita kiasi na ubovu wa boti zenyewe. 

Katika ajali nyingine ya Aprili 15 katika Ziwa Kivu wakati wa safari ya Goma kuelekea Kalehe, watu zaidi ya 25 walithibitishwa kupoteza maisha huku wengine zaidi ya 100 wakitoweka.