Waasi wa Nigeria watishia kushambulia taasisi za mafuta
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i5401-waasi_wa_nigeria_watishia_kushambulia_taasisi_za_mafuta
Waasi wa eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta nchini Nigeria wametishia kwamba watazidisha mashambulizi yao dhidi mabomba na taasisi za mafuta ya petroli nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 19, 2016 11:51 UTC
  • Waasi wa Nigeria watishia kushambulia taasisi za mafuta

Waasi wa eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta nchini Nigeria wametishia kwamba watazidisha mashambulizi yao dhidi mabomba na taasisi za mafuta ya petroli nchini humo.

Kundi linalojiita Walipizaji Kisasi wa Niger Delta limetoa taarifa likimkosoa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ambaye limesema anajali visima vya mafuta kuliko maisha ya wakazi wa Niger Delta. Kundi hilo pia limetangaza kuwa ndilo lililoshambulia mabomba ya mafuta chini ya bahari hapo mwezi Februari mwaka huu. Shambulizi hilo liliilazimisha kampuni kubwa ya mafuta ya Shell kusimamisha uuzaji nje bidhaa hiyo kwa wiki kadhaa.

Siku chache zilizopita Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria alisema kuwa atakabiliana vikali na watu waovu wanaoharibu mabomba ya mafuta ya petroli.