Jeshi Algeria launga mkono kuanza mazungumzo ya kitaifa
Kamanda wa jeshi la Algeria ametangaza kuwa anaunga mkono kuanza mazungumzo jumuishi ya kitaifa yatakayosimamiwa na shakhia wanaojitegemea.
Ahmed Qaid Saleh ameunga mkono pendekezo la Rais wa muda wa Algeria Abdulqadir bin Saleh kwa ajili ya kuanza mazungumzo mapana ya kitaifa. Mazungumzo hayo yatahudhuriwa na shakhsiya wa kujitegemea. Awali Bin Saleh alikuwa ametangaza habari ya kuanzishwa kundi maalumu la kuandaa mazingira mazuri ya kufanyika uchaguzi wa rais nchini Algeria.
Algeria imekumbwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa tangu baada ya kuanza maandamano ya mitaani Februari 22 mwaka huu.
Kwa mujibu wa katiba ya Algeria, Bin Saleh ambaye alichukua madaraka ya nchi tangu Aprili 9 mwaka huu, wiki moja baada ya kujiuzulu Rais Abdulaziz Bouteflika kutokana na mashinikizo na maandamano ya wananchi wa nchi hiyo, alipasa kuondoka madarakani tarehe 9 mwezi huu wa Julai. Hata hivyo kiongozii huyo amesema kuwa ataendelea kukalia kiti hicho hadi utakapofanyika uchaguzi mpya wa rais.