Watu 12 wauawa katika mashambulio ya wanamgambo wa ADF huko DRC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i54949-watu_12_wauawa_katika_mashambulio_ya_wanamgambo_wa_adf_huko_drc
Watu 12 wameuawa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiwemo watoto wawili kufuatia mashambulio ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la ADF la Uganda.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 23, 2019 10:00 UTC
  • Watu 12 wauawa katika mashambulio ya wanamgambo wa ADF huko DRC

Watu 12 wameuawa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiwemo watoto wawili kufuatia mashambulio ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la ADF la Uganda.

Duru za usalama zinasema kuwa, raia hao wameuawa kufuatia mashambulio mawili ya wanamgambo hao yaliyofanywa usiku wa kuamkia Jumatatu na kwamba, makumi ya watu wamejeruhiwa katika mashambulio hayo.

Baadhi ya ripoti zinaeleza kuwa, wanachama wa kundi hilo la kigaidi wametekeleza mashambulio ya usiku katika mji wa Beni na kuwaua watu kwa kuwapiga risasi.

Makumi ya watu inasemekana wameyakimbia makazi yao baada ya mashambulio hayo wakihofia usalama wa maisha yao.

Waasi wa ADF wa Uganda wanaoendesha harakati zao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Waasi wa Uganda wa ADF wa Uganda walianzisha harakati zao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwaka 1994 na katika miaka hiyo yote wameuwa mamia ya raia wa eneo hilo na kusababisha kuzorota usalama katika maeneo hayo.

Maeneo ya katikati, mashariki na kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanakabiliwa na ukosefu wa amani kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Kushindwa jeshi la DRC na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kukabiliana na waasi na makundi ya wanamgambo wenye silaha katika nchi hiyo kumepelekea kuongezeka hali ya mchafukoge na ukosefu wa amani nchini humo.