Vyama vya upinzani Algeria vyatoa wito wa uasi wa kiraia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i55161-vyama_vya_upinzani_algeria_vyatoa_wito_wa_uasi_wa_kiraia
Vyama vya upinzani nchini Algeria vimetoa wito wa kufanyika uasi wa kiraia nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 03, 2019 07:37 UTC
  • Vyama vya upinzani Algeria vyatoa wito wa uasi wa kiraia

Vyama vya upinzani nchini Algeria vimetoa wito wa kufanyika uasi wa kiraia nchini humo.

Walgeria waliofanya maanamano makubwa jana Ijumaa chini ya hatua kali za kiusalama wameitaka serikali kujibu matakwa yao na kutangaza kuwa, wataendeleza maandamano na malalamiko yao kupitia uasi wa kiraia. 

Watu walioshiriki katika maandamano ya Ijumaa ya jana katika miji mbalimbali ya Algeria wametaka kuondoka madarakani maafisa wa utawala wa zamani Abdelaziz Bouteflika na kuanzishwa mazungumzo yatakayoshirika makundi yote.

Wito huo umetolewa baada ya kamati ya mazungumzo ya kitaifa iliyoundwa nchini humo juma lililopita kukumbana na matatizo mengi. Kamati hiyo inayoundwa na wajumbe sita inaongozwa na  Karim Younes aliyekuwa Spika wa Bunge la Algeria, na baadhi ya makundi ya wananchi nchini humo yana wasiwasi kuhusu muundo wake na uhuru wa kazi zake mkabala wa serikali ya muda ya nchi hiyo. 

Maandamano ya wananchi wa Algeria

Maandamano ya wananchi wa Algeria yalianza baada ya aliyekuwa rais wa nchi, Abdelaziz Bouteflika kutangaza nia yake ya kugombea kiti hicho kwa mara ya tano mfululizo. Maandamano ya Waalgeria yalimlazimisha Bouteflika kung'atuka baada ya kuiongoza Algeria kwa zaidi ya miaka 20 na madaraka ya nchi hiyo sasa yako mikononi mwa Spika wa Bunge Abdul Qadir Bin Saleh.