Uganda yawatia mbaroni watu 16 kwa kushiriki vitendo vya ubaradhuli
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i56827-uganda_yawatia_mbaroni_watu_16_kwa_kushiriki_vitendo_vya_ubaradhuli
Serikali ya Uganda imewatia mbaroni wanaharakati 16 kwa tuhuma za kushiriki vitendo vya ubaradhuli nchini humo.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Oct 24, 2019 13:14 UTC
  • Polisi wa Uganda
    Polisi wa Uganda

Serikali ya Uganda imewatia mbaroni wanaharakati 16 kwa tuhuma za kushiriki vitendo vya ubaradhuli nchini humo.

Msemaji wa Polisi ya Uganda, Patrick Onyango ameviambia vyombo vya habari kuwa, washukiwa hao wamefanyiwa vipimo na imethibiti kuwa walishiriki ufuska huo ambao hukumu yake ni kifungo cha maisha jela.

Wanaume hao wenye kati ya umri wa miaka 22 hadi 35 wanatazamiwa kupandishwa kizimbani mara tu uchunguzi utakapokamilika, wakiandamwa na shitaka la kushiriki uchafu huo ulio kinyume na sheria na maumbile.

Haya yanajiri siku chache baada ya serikali ya Kampala kutangaza nia yake ya kurejesha muswada bungeni ambao utatoa adhabu kali kwa mabaradhuli na wanaoendesha vitendo vichafu vya mahusiano ya watu wenye jinsia moja.

Ramani ya Uganda

Muswada huo ambao huko Uganda unajulikana kwa jina maarufu la “Ua Mabaradhuli” ulikataliwa bungeni miaka mitano iliyopita kutokana na matatizo ya kiufundi. Hata hivyo mapema mwezi huu serikali ya Uganda ilisema kuwa ina mpango wa kuurejesha bungeni katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Serikali ya Uganda inasema vitendo hivyo vichafu vimeenea sana nchini humo na inabidi sheria kali ziwekwe kudhibiti ngono hizo zilizo kinyume na maumbile.