SAUTI, Wafanyabiashara wa Uganda: Rwanda bado haijatufungulia kikamilifu mpaka wake
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i57369-sauti_wafanyabiashara_wa_uganda_rwanda_bado_haijatufungulia_kikamilifu_mpaka_wake
Wafanyabiashara wa Uganda wameendelea kulalamikia hatua ya serikali ya Rwanda ya kutofungua kikamilifu mipaka yake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 19, 2019 12:33 UTC

Wafanyabiashara wa Uganda wameendelea kulalamikia hatua ya serikali ya Rwanda ya kutofungua kikamilifu mipaka yake.

Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao, licha ya serikali za Kampala na Kigali kutia saini mkataba wa kuwasahilishia wafanyabiashara wa pande mbili katika mipaka yao, lakini bado upande wa Rwanda umekuwa mgumu kwa raia wa Uganda wanaoingiza na kutoa biashara zao nchi hiyo.

Licha ya marais wa nchi mbili kutiliana saini makubaliano ya kibiashara, lakini bado hali haijaboreka

Hii ni katika hali ambayo wafanyabiashara wa Uganda wamepongeza huduma zinazotolewa na bandari ya Dar es Salaam, Tanzania ingawa wamelalamika umbali uliopo kati ya nchi mbili.

Jiunge na mwandishi wetu wa mjini Kampala, Kigozi Ismail kwa taarifa kamili, lakini bonyeza juu kwenye alama ya sauti…………/