Ireland yaweka sheria ya kuwawajibisha mawakili Waislamu kuapa kwa kutumia Qur'ani
(last modified Mon, 25 Apr 2016 04:05:18 GMT )
Apr 25, 2016 04:05 UTC
  • Ireland yaweka sheria ya kuwawajibisha mawakili Waislamu kuapa kwa kutumia Qur'ani

Jamii ya wanasheria nchini Ireland, imewawajibisha mawakili na washauri wa sheria Waislamu kutumia Qur'ani Tukufu wakati wa kula kiapo.

Gazeti la Sunday Independent limeripoti kuwa, Peter Kelly, Jaji wa Mahakama Kuu ya Ireland ametoa amri ya kuwawajibisha mawakili nchini humo kuapa kwa kutumia vitabu vyao vitakatifu.

Kabla ya hapo jamii ya wanasheria wa Ireland ilikuwa imewataka kwa siri wanachama wake wahakikishe kuwa wanapokula viapo wanatumia vitabu vyao vitakatifu.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, Wakristo na Mayahudi nao wanatakiwa kula viapo kwa kutumia vitabu vyao.

Takwimu zinaonesha kuwa, hadi mwaka 2013, Ireland ilikuwa na karibu watu milioni nne na nusu huku idadi ya Waislamu ikiwa ni zaidi ya 50 elfu.

Tags