WHO: Watu milioni 50 wanakabiliwa na matatizo ya kisaikolojia Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i57890-who_watu_milioni_50_wanakabiliwa_na_matatizo_ya_kisaikolojia_nigeria
Shirika la Afya Duniani WHO) limesema mamilioni ya wananchi wa Nigeria wanakabiliwa na tatizo moja au jingine la kiakili.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Dec 15, 2019 04:15 UTC
  • WHO: Watu milioni 50 wanakabiliwa na matatizo ya kisaikolojia Nigeria

Shirika la Afya Duniani WHO) limesema mamilioni ya wananchi wa Nigeria wanakabiliwa na tatizo moja au jingine la kiakili.

WHO imesema, katika kila watu wanne nchini Nigeria, mmoja anaandamwa na tatizo la kisaikolojia. Huko ni kusema kuwa, zaidi ya Wanigeria milioni 50 wana matatizo ya kiakili.

Kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la Afya Duniani, Nigeria ambayo ni nchi ya saba kwa ukubwa barani Afrika ndiyo inaongoza kwa kuwa na kesi nyingi za watu wanaokabiliwa na msongo wa mawazo, na pia ni taifa la 15 kwa kurekodi visa vingi vya watu kujitoa uhai duniani.

Takwimu za Wizara ya Afya ya nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika zinaonesha kuwa, kuna madaktari 150 tu wa kushughulikia matatizo ya kiakili na kisaokolojia nchini Nigeria, nchi ambayo ina jamii ya watu milioni 200.

Vijana ndio wahanga wakuu wa matatizo ya kiakili na msongo wa mawazo

WHO inasema ni asilimia 10 tu ya Wanigeria wanaokabiliwa na matatizo hayo ya kiakili ndio wanapata huduma za matibabu huku aghalabu wakikosa huduma hizo ama kutokana na uhaba wa madaktari wa magonjwa hayo au ukosefu wa fedha za kulipia matibabu yenyewe.

Kwa mujibu wa Baraza Kuu la Madaktari la Uingereza, kwa akali madaktari 12 huondoka Nigeria kila wiki kwenda kusaka ajira katika nchi hiyo ya Ulaya.