Watu 23 wapoteza maisha wakigombania chakula Niger
(last modified Tue, 18 Feb 2020 07:57:13 GMT )
Feb 18, 2020 07:57 UTC
  • Watu 23 wapoteza maisha wakigombania chakula Niger

Kwa akali watu 23 wameuawa katika mkanyagano wa kugombania chakula cha msaada nchini Niger.

Duru za habari zinaarifu kuwa, tukio hilo la kukanyagana lililotokea jana Jumatatu katika mkoa wa Diffa, kaskazini mashariki mwa Niger, ambapo wakimbizi walikuwa wakigombania chakula na nguo za msaada.

Mashuhuda wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, Mkuu wa Jimbo la Babagana la Nigeria, Oumara Zulum alifanya ziara katika nchi hiyo jirani kwa lengo la kugawa chakula cha msaada kwa wakimbizi wa Nigeria.

Niger ni moja ya nchi maskini zaidi duniani

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, eneo hilo lina wakimbizi zaidi ya 250,000. Aghalabu ya wakimbizi hao ni wale waliotoroka vita na mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Kundi hilo la ukufurishaji limekuwa likifanya hujuma za kikatili katika nchi za Niger, Nigeria, Chad na Cameroon, mashambulio ambayo hadi sasa yameshapelekea makumi ya maelfu ya watu kuuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi hizo za Afrika Magharibi.

Tags