Watu 29 wauawa katika shambulio la kigaidi nchini Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i60160-watu_29_wauawa_katika_shambulio_la_kigaidi_nchini_nigeria
Kwa akali watu 29 wameuawa katika shambulio la kigaidi nchini Nigeria na makumi ya wengine kujeruhiwa.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Apr 04, 2020 03:19 UTC
  • Watu 29 wauawa katika shambulio la kigaidi nchini Nigeria

Kwa akali watu 29 wameuawa katika shambulio la kigaidi nchini Nigeria na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Vyombo vya usalama vya Nigeria vimetangaza kuwa, watu waliokuwa na silaha wamefanya mashambulio dhidi ya maeneo mawili kaskazini na mashariki mwa Nigeria na kuua kwa akali raia 29 na kuwajeruhi makumi ya wengine.

Muhammadu Saad Abubakar, Mkuu wa Usalama wa Taifa  katika jimbo la Sokoto ameziambia duru za habari kwamba,  mashambulio hayo yametekelezwa na watu kadhaa waliokuwa wamepanda pikipiki.

Wapanda pikipiki hao walipowasili katika maeneo hayo walianza kuwashambulia kwa risasi kiholela wakazi wa maeneo hayo, imeeleza taarifa iliyotolewa na Muhammadu Saad Abubakar, Mkuu wa Usalama wa Taifa  katika jimbo la Sokoto.

Jimbo la Sokoto limekuwa likishuuhudia mashambulio kama hayo mara kwa mara na kuhatarisha usalama wa raia.

Wanamgambo wa Boko Haram

Maeneo hayo yanakabiliwa na ukosefu wa usalama katika hali ambayo, Nigeria na hasa maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika yamekuwa yakikabiliwa na mashambulio ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram.

Kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa, katika muongo mmoja wa shughuli za kundi la Boko Haram nchini Nigeria, zaidi ya watu elfu 30 wameuawa na wengine wanaokaribia milioni tatu wamekuwa wakimbizi.

Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram lilianzisha shughuli zake za kigaidi mwaka 2009 kaskazini mwa Nigeria ambapo hadi sasa limepanua wigo wake hadi katika nchi za Niger, Chad na kaskazini mwa Chad.