Maandamano wa wapinzani wa el Sisi yafanyika nchini Misri
Baadhi ya wananchi wa Misri wamefanya maandamano katika mji wa Suez wa mashariki mwa mji mkuu Cairo kupinga siasa za rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah el Sisi.
Gazeti la al Quds al Arabi limetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, maandamano hayo yalifanyika jana Ijumaa katika eneo la Arab el Ma'mal mjini Suez.
Waandamanaji hao wametaka kupinduliwa serikali ya Abdel Fattah el Sisi lakini polisi wa Misri walikandamiza maandamano hayo na kuwatia mbaroni baadhi ya waandamanaji.
Sababu kuu ya maandamano hayo ni hali mbaya ya kiuchumi iliyoko nchini Misri na waandamanaji walipata nguvu za kushiriki kwenye maandamano hayo baada ya kuenea mkanda wa video unaoonesha ufisadi na ubadhirifu mkubwa unaofanywa na el Sisi na baadhi ya viongozi wa Misri.
Maandamano hayo ni muendelezo wa wimbi la maandamano yaliyoanzia mwezi Septemba 2019 na serikali ya Misri imeweka sheria kali za kudhibiti vyombo vya habari vya nje na waandishi wa habari wanaoakisi matukio kama hayo.
Shirika la Kimataifa la Amnesty International limesema kwamba, watu elfu mbili wametiwa maandamano hayo.