UN: Mashambulizi ya Saudia yanalenga raia Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i64-un_mashambulizi_ya_saudia_yanalenga_raia_yemen
Kamati ya wataalamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa Saudi Arabia na waitifaki wake wamekiuka haki za binadamu na sheria za kimataifa katika uvamizi na mashambulizi yao dhidi ya Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 27, 2016 05:32 UTC
  • UN: Mashambulizi ya Saudia yanalenga raia Yemen

Kamati ya wataalamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa Saudi Arabia na waitifaki wake wamekiuka haki za binadamu na sheria za kimataifa katika uvamizi na mashambulizi yao dhidi ya Yemen.

Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa wamesema mashambulizi ya anga ya Saudia yamekuwa yakilenga maeneo ya raia; jambo linalokinzana na sheria za kimataifa na linalohesabiwa kuwa jinai za kivita. Kamati hiyo ya wataalamu ya UN imetaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchunguza suala hilo na kuwatambua wahusika wakuu na kisha kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria.

Ripoti ya kamati hiyo ya wataalamu imesema kuwa Saudi Arabia imetekeleza mashambulizi 120 yanayohesabiwa kuwa jinai dhidi ya binadamu kwa kuwa yamelenga mabasi ya umma, shule, maeneo ya ibada, hospitali na taasisi za Umoja wa Mataifa katika maeneo mbalimbali ya Yemen.

Saudia iliivamia Yemen tangu mwezi Machi mwaka uliopita na takwimu zinaonyesha kuwa hadi sasa karibu watu 10 000 wameuawa na wengine 16 000 wamejeruhiwa huku makumi ya maelfu ya wengine wakiachwa bila makao. Wengi wa wahanga wa hujuma za Saudi Arabia nchini Yemen ni wanawake na watoto wadogo.