Sudan yazidi kuandamwa na mashinikizo ili ianzishe uhusiano na utawala wa Kizayuni
(last modified Tue, 20 Oct 2020 12:04:33 GMT )
Oct 20, 2020 12:04 UTC
  • Sudan yazidi kuandamwa na mashinikizo ili ianzishe uhusiano na utawala wa Kizayuni

Waziri wa Habari wa Sudan amefichua kuwa, nchi hiyo inaandamwa na mashiniklizo ili ianzishe uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Akizungumza na televisheni ya al Jazeera Faisal Mohamed Saleh amefichua kuwa Sudan inakabiliwa na mashinikizo makubwa ili ianzishe mchakato wa kufikia mapatano ya kuanzisha uhusiano na Israel. Waziri wa Habari wa Sudan amebainisha hayo baada ya kuondolewa jina la Sudan katika orodha ya Marekani ya nchi eti zinazounga mkono ugaidi. 

Tangu mwaka mmoja uliopita Sudan ilikuwa ikifanya juhudi ili kutoka katika orodha nyeusi ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani. 

Itakumbukwa kuwa, katika mazungumzo ya wiki jana kati ya wawakilishi wa mazungumzo wa Marekani, Sudan na Abu-Dhabi; upande wa Marekani ulisema kuwa Sudan inapasa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni kama sharti la kuiondoa nchi hiyo katika orodha nyeusi ya Marekani ya nchi eti zinazounga mkono ugaidi. 

Wananchi na makundi ya Sudan yanapinga kuanzishwa uhusiano kati ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni. 

Maandamano ya Wasudani ya kupinga kuanzishwa uhusiano kati ya nchi yao na Israel 

 

Tags