Wananchi wa Nigeria watoa ushahidi kuhusu jinai za jeshi la nchi hiyo
Kamati ya Mahakama ya Nigeria imeripoti kuwa, raia wa nchi hiyo wamewasilisha ushahidi wao wa kimaandishi kuhusu jinai na uhalifu uliofanywa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya raia.
Kamati hiyo ya Mahakama ya Nigeria imetangaza kuwa wananchi hao wametoa uhahidi wao kuhusu jinai na ufyatuaji risasi uliofanywa na jeshi la taifa dhidi ya raia katika mji wa Lagos.
Kwa mujibu wa ushuhuda uliotolewa na watu hao, askari wa jeshi la Nigeria mwezi Oktoba mwaka huu waliwafyatulia risasi waandamanaji katika mji wa Lagos na kisha kuiweka miili ya watu iliyowauwa ndani ya malori na kuipeleka kusikojulikana.
Kamati ya Mahakama ya Nigeriia tayari imeanza uchunguzi kuhusu ushahidi huo uliotolewa na wananchi kuhusu jinai na ufyatuaji risasi wa jeshi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakilalamikia ukandamizaji wa polisi. Jeshi na polisi ya Nigeria kwa upande wao wamekanusha kutekeleza mauaji hayo dhidi ya waandamanaji. Maandamano ya wananchi huko Nigeria yalianza tarehe 30 mwezi Oktoba mwaka huu.
Ripoti ya Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International inaeleza kuwa, wanajeshi na askari polisi wa Nigeria waliwaua waandamanaji wasiopungua 12 katika maandamano hayo.