Wagombea wa wizara mbalimbali Sudan watangazwa
Baraza la uongozi la Sudan limetangaza kuwa limemkabidhi Waziri Mkuu wa nchi hiyo orodha ya majina ya wagombea wa nafasi za uwaziri nchini humo.
Mariam Sadiq al Mahdi Msemaji wa Baraza la Uongozi la Sudan ametangaza kuwa, wajumbe wa baraza hilo wamefanya kikao kilichoongozwa na Abdulfattah al Burhan Mkuu wa baraza hilo katika ikulu ya rais huko Khartoum mji mkuu wa nchi hiyo.
Amesema katika kikao hicho wajumbe walikubaliana kuwa, jana Jumatatu orodha hiyo ya majina ya wagombea wa nafasi za uwaziri ikabidhiwe kwa Waziri Mkuu Abdallah Hamduk ili serikali ya mpito ya Sudan iweze kutangazwa hadi kufikia Alhamisi wiki hii.
Bi Mariam Sadiq al Mahdi ameongeza kuwa, kikao cha Khartoum kimejadili pia mchakato wa kukamilisha mapatano kwa jaili ya kuunda taasisi za serikali ya mpito.
Sudan inaunda serikali mpya kufuatia mapatano ya amani yaliyofikiwa miezi kadhaa iliyopita kati ya Khartoum na makundi kadhaa yanayobeba silaha. Aidha Novemba mwaka jana baraza la uongozi la Sudan na serikali ya nchi hiyo ziliifanyia marekebishoo hati yakatiba ya nchi hiyo ambapo kwa mujibu wake marhala ya kipindi cha mpito kimeongezwa muda wa karibu miezi 14.