Amnesty International yakosoa kuibuliwa anga ya vitisho na ukandamizaji huko Sudan Kusini
(last modified Tue, 02 Feb 2021 11:13:21 GMT )
Feb 02, 2021 11:13 UTC
  • Amnesty International yakosoa kuibuliwa anga ya vitisho na ukandamizaji huko Sudan Kusini

Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International limetangaza kuwa idara ya usalama wa taifa ya Sudan Kusini inatumia mamlaka iliyonayo kuibua vitisho na hofu miongoni mwa waandishi habari, wanaharakati na wakosoaji wa serikali; jambo linaloibua hali ya wasiwasi nchini humo.

Kitengo cha Amnesty International mashariki na kusini mwa Afrika kimeripoti kuwa, kutolewa vitisho vya kufuatiliwa vikali ni moja ya silaha zinazotumiwa na Idara ya Usalama wa Taifa ya Sudan Kusini dhidi ya watu hao tajwa. Wakati huo huo wakosoaji wa serikali ya Sudan Kusini na waharakati wa haki za binadamu nchini humo wamesema kuwa kila siku wanaishi katika hali ya hofu ya kufanyiwa ujasusi.   

Amnesty International imeongeza kuwa, ilifanya uchunguzi kwa muda wa miaka miwili ambapo ilifanya mahojiano na wanaharakati 63, waandishi habari na mawakili huko Sudan Kusini. Amnesty International aidha ilichunguza zaidi ya ripoti 57 na tafiti zilizoandaliwa na majopo mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na taasisi za kimataifa za serikali na zisizo za kiserikali mbali na kuchunguza maazimio na sheria nyinginezo.  

Ripoti ya Amnesty International inaeleza kuwa, serikali ya Sudan Kusini inaitumia Idara ya Usalama wa Taifa ya nchi hiyo kuibua hofu, utumiaji mabavu, kutesa watu, kutia mbaroni raia kiholela, kuwaweka watu kizuizini kwa muda mrefu na kutekeleza mauaji kinyume cha sheria ili kuwanyamazisha wakosoaji wa serikali, watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari nchini humo. 

Kuweka kizuizini watu kwa muda mrefu moja ya mateso ya Idara ya Usalama wa Taifa ya Sudan Kusini  

 

Tags