Ethiopia yaahirisha tena uchaguzi kwa sababu za kiusalama, changamoto za vifaa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i70192-ethiopia_yaahirisha_tena_uchaguzi_kwa_sababu_za_kiusalama_changamoto_za_vifaa
Ethiopia imechelewesha tena uchaguzi wa kitaifa baada ya baadhi ya vyama vya upinzani kusema kuwa, vitasusia uchaguzi huo ambao pia hautafanyika katika eneo la Tigray kutokana na mzozo unaendelea katika eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 16, 2021 03:31 UTC
  • Ethiopia yaahirisha tena uchaguzi kwa sababu za kiusalama, changamoto za vifaa

Ethiopia imechelewesha tena uchaguzi wa kitaifa baada ya baadhi ya vyama vya upinzani kusema kuwa, vitasusia uchaguzi huo ambao pia hautafanyika katika eneo la Tigray kutokana na mzozo unaendelea katika eneo hilo.

Birtukan Mideksa, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uchaguzi ya Ethiopia (NEBE), amesema kwamba, ucheleweshaji wa kufungua vituo vya kupigia kura na usajili wa wapigakura vimepelekea kuahirishwa siku ya uchaguuzi mkuu.

Mideksa ametaja mambo kadhaa kuwa ndiyo sababu ya kucheleweshwa zoezi hilo ikiwa ni pamoja ucheleweshwaji wa vifaa, kutokamilika zoezi la kuandikisha wapigakura, kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa uchaguzi, kuchapa na kusambaza karatasi za kura.

Awali uchaguzi mkuu nchini Ethiopia ulipangwa kufanywa mwezi Agosti mwaka jana lakini uliahirishwa kwa mara ya kwanza kwa sababu ya janga la corona.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ambaye alianzisha mageuzi makubwa ya kisiasa baada ya kuchukua madaraka mnamo 2018 na kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka uliofuata, ameahidi mara kadhaa kwamba uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki.