Wanajeshi wa Ethiopia wamejizatiti katika mipaka ya mashariki mwa Sudan
(last modified Thu, 10 Jun 2021 02:31:18 GMT )
Jun 10, 2021 02:31 UTC
  • Wanajeshi wa Ethiopia wamejizatiti katika mipaka ya mashariki mwa Sudan

Maafisa wa kijeshi wa Sudan wameripoti kuwa, wanajeshi wa Ethiopia wamekusanyika katika mipaka ya nchi hiyo na Sudan.

Maafisa hao wameeleza kuwa, wanajeshi wa Ethiopia wamejizatiti vilivyo katika eneo la Amhara la kaskazini mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa mashariki wa Sudan huku wakiwa na zana nzito za kijeshi; na wamekaribia kambi za jeshi za nchi hiyo.

Hii ni katika hali ambayo jeshi la Sudan pia limetuma askari katika mipaka ya kimataifa na kuweka kambi katika eneo la mpakani mashariki mwa Sudan. Sudan imesema kuwa imechukua hatua hiyo ili kuwazuia wakulima na wanamgambo wa Kiethiopia kuingia nchini humo.  

Mzozo wa eneo la al Fashaga kati ya Sudan na Ethiopia 

 Sudan na Ethiopia zinahitilafiana kuhusu ardhi ya kilimo katika eneo la al Fashaga kwenye mpaka wa kimataifa wa Sudan; eneo ambalo wakulima wa Kiethiopia wamekuwa wakiishi hapo kwa miaka kadhaa sasa. 

Wanamgambo wa Kiethiopia karibu miaka 26 iliyopita walivamia ardhi za wakulima wa Sudan katika eneo hilo la al Fashaga na kisha wakawatoa kwa nguvu katika mashamba yao kwa kutumia silaha na kuzidhibiti ardhi hizo.

Khartoum inalituhumu jeshi la Ethiopia kuwa linawaunga mkono wanangambo hao.  

Tags