Kamanda wa Jeshi la Sudan amfuta kazi mwendesha mashtaka wa nchi hiyo
(last modified Mon, 01 Nov 2021 16:08:25 GMT )
Nov 01, 2021 16:08 UTC
  • Mubarak Mahmod
    Mubarak Mahmod

Abdel Fattah al Burhan Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Sudan amemfuta kazi mwendesha mashtaka na mahakimu wengine saba wa nchi hiyo.

Abdel Fattah al Burhan amemfuta kazi Mubarak Mahmod Mwendesha Mashtaka wa nchi hiyo baada ya kuchukua uamuzi wa kuwaachia huru viongozi kadhaa wa utawala wa Rais qwa zamani wa Sudan Omar al Bashir aliyeondolewa madarakani Aprili mwaka 2019. 

Taarifa zinasema kuwa, kamanda wa jeshi la Sudan ameagiza pia kurudishwa jela maafisa wa utawala wa al Bashir walioachiwa huru na Mubarak Mahmoud. 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi iliyopita lilitoa taarifa na kutangaza kuwa, nchi wanachama wa baraza hilo linatiwa wasiwasi na mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini Sudan Oktoba 25 mwaka huu, kusitishwa shughuli za taasisi kadhaa za mpito na kutangazwa hali ya hatari baada ya kuwekwa kizuizini Waziri Mkuu wa nchi hiyo. Baraza la Usalama liliongeza kuwa linatiwa wasiwasi  pia na kutiwa mbaroni viongozi wa kiraia wa serikali ya mpito ya Sudan.  

Wiki iliyopita, vyombo vya habari vilitangaza habari ya kujiri mapinduzi ya kijeshi huko Sudan na kuwekwa kizuizini Waziri Mkuu, Abdallah Hamdok na mawaziri wengine kadhaa wa serikali ya mpito ya nchi hiyo. Aidha masaa kadhaa baada ya mapinduzi hayo ya kijeshi Al Burhan alitangaza hali ya hatari huko Sudan na kuvunjwa Baraza la Uongozi la nchi hiyo ambalo yeye ndiye Mwenyekiti.  

Abdallah Hamdo, Waziri Mkuu wa Sudan aliyepinduliwa na jeshi 

 

Tags