Wakimbizi wa Burundi waongezeka Tanzania
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i805-wakimbizi_wa_burundi_waongezeka_tanzania
Wakimbizi zaidi kutoka Burundi wanazidi kumiminika Tanzania kutokana na kuzidi kutokota mgogoro wa kisiasa katika nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 07, 2016 22:17 UTC
  • Wakimbizi wa Burundi waongezeka Tanzania

Wakimbizi zaidi kutoka Burundi wanazidi kumiminika Tanzania kutokana na kuzidi kutokota mgogoro wa kisiasa katika nchi hiyo.

Ripoti zinasema wakimbizi Warundi zaidi ya 110,000 walioko katika kambi ya NarugusuTanzania wanakabiliwa na hatari ya kupoteza maisha kutokana na kipindupindu kufuatia mvua kubwa na mafuriko kambini.

Mashirika ya kutoa misaada yanasema yanahofia mripuko wa kipindupindu ambacho kiliua wakimbizi 33 wa Burundi mwezi Mei kutokana na mvua kubwa na ukosefu wa vyoo safi.

Mashirika ya kutoa misaada ya Oxfam, Save the Children na HelpAge International yametoa taarifa na kusema mamia ya wakimbizi wanaingia Tanzania kila siku.

Takribani watu laki mbili wamekimbia Burundi tokea mwezi Aprili mwaka jana kufuatia mgogoro ulioibuka nchini humo baada ya Rais Pierre Nkrunzziza kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu mfululizo. Nkurunziza alishinda uchaguzi huo wa mwezi Julai na hadi wakati huu nchi hiyo, hasa mji mkuu Bujumbura, umekuwa ukishuhudia machafuko na mauaji ya mara kwa mara.